Saturday, June 13, 2020

AWAMU YA TANO NA FURSA ZA NAFAKA



FURSA ZA UWEKEZAJI KWA WADAU WA NAFAKA, TANZANIA 

Zimetayarishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imeandaa Miongozo ya Uwekezaji1 ya Mikoa kwa lengo la kuonesha (kuibua) fursa za uwekezaji zilizopo katika mikoa husika na kuwavutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi. Miongozo hii ya Uwekezaji inalenga kuwavutia wawekezaji kuwekeza katika mikoa husika ili kusaidia ukuaji wa biashara na uwekezaji nchini. (Mpaka sasa Miongozo ya Uwekezaji iliyoandaliwa ni ya Mikoa ya: Simiyu, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma, Manyara, Tanga, Kigoma, Songwe, Katavi, Ruvuma, Kagera, Geita na Pwani. Yafuatayo ni maelezo mafupi ya fursa za uwekezaji katika sekta ya nafaka yatakayosaidia wawekezaji kuchangamkia fursa hizo katika mikoa husika nchini Tanzania. 1. UJENZI WA MAGHALA Muhtasari wa Fursa Mambo Muhimu  Mfumo wa Maghala Tanzania kwa ujumla wake bado hautoshelezi  Maghala yaliyopo sasa hayatoshi na mengi yana viwango duni kiasi cha kuathiri usalama wa chakula na hivyo kuongeza upotevu wa mazao baada ya mavuno  Uimarishaji wa Mfumo wa Maghala Tanzania ni jambo muhimu na la haraka, hivyo wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika ujenzi wa Maghala mapya yenye viwango vinavyokubalika. Hii itasaidia usambazaji wa nafaka katika maeneo yenye upungufu. Maeneo kwa ajili ya Uwekezaji  Mikoa ya Mwanza, Tanga, Kilimanjaro, Kagera, Ruvuma, Simiyu, Katavi na Dodoma Msaada uliopo  Usalama na utoshelevu wa chakula ni moja ya vipaumbele vya Taifa. Serikali imeendelea kushirikiana na sekta binafsi kutatua changamoto za usalama na utoshelevu wa chakula nchini. Ili kufanikisha hili, Serikali ya Tanzania imeendelea kuweka mazingira bora ya biashara katika sekta ya kilimo ikiwemo kufuta tozo kandamizi na kupunguza muda wa kupata leseni. Aidha, Serikali Kuu inahimiza mazungumzo na wafanya biashara kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto na kero zao. 2. BIASHARA YA MIPAKANI Muhtasari wa Fursa Mambo Muhimu  Mikoa inayopakana na nchi jirani inafaa kwa ujenzi wa masoko na maghala hasa mipakani. Miundombinu hiyo ni muhimu katika kuchochea biashara kati ya Tanzania na nchi jirani  Wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika miundombinu ya masoko na maghala mipakani kwakuwa uhitaji ni mkubwa na biashara mipakani ni kubwa Maeneo kwa ajili ya Uwekezaji  Mikoa ya Kagera, Kigoma, Mara, Mwanza, Tanga, Kilimanjaro, Ruvuma, na Rukwa Msaada uliopo  Serikali imetoa kipau mbele katika kusimamia uwiano mzuri kati ya utoshelevu wa chakula na uuzaji mazao nje ya nchi. 3. KUWEKEZA KATIKA MAENEO MAALUM YA KIUCHUMI (SPECIAL ECONOMIC ZONES) Muhtasari wa Fursa Mambo Muhimu  Mikoa mingi nchini Tanzania imetenga maeneo maalum ya kiuchumi kwa ajili ya uwekezaji jumuishi (Special Economic Zones) na hivyo kuna fursa kubwa ya kujenga maghala katika maeneo hayo  Wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika ujenzi wa maghala ya kisasa katika maeneo maalum ya kiuchumi ndani ya mikoa husika. Uwekezaji huu utasaidia kuhifadhi nafaka kwa wingi na hivyo kusaidia biashara na nchi jirani Maeneo kwa ajili ya Uwekezaji  Mikoa ya Kagera, Simiyu, Pwani,Kigoma na Geita Msaada uliopo  Serikali imeweka kipaumbele katika kuendeleza maeneo maalum ya kiuchumi kama njia ya kuchochea biashara na kadhalika. 1 Tembelea http://www.esrf.or.tz/invest.php 4. USAFIRISHAJI WA NAFAKA Muhtasari wa Fursa Mambo Muhimu  Fursa zipo nyingi katika usafirishaji wa nafaka kutoka maeneo yenye akiba kwenda maeneo yenye upungufu ndani na nje ya nchi kama vile Malawi, Kongo, Zimbabwe, Uganda, Kenya, Sudani ya Kusini, na Zambia  Wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika usafirishaji wa nafaka ili kutatua changamoto ya upungufu wa chakula kwa baadhi ya maeneo na kuchochea biashara ya nje Maeneo kwa ajili ya Uwekezaji  Mikoa ya Ruvuma, Katavi, Rukwa, Geita, Pwani, Dodoma, Simiyu na Songwe. Msaada uliopo  Serikali imeweka mazingira bora na rahisi ya upatikanaji wa leseni za usafirishaji na leseni za biashara kwa ujumla. 5. UCHAKATAJI WA NAFAKA Muhtasari wa Fursa Mambo Muhimu  Uhitaji wa nafaka bora iliyochakatwa (mahindi, mtama, uwele, na mpunga) nchini umeendelea kuongezeka. Masoko ya nafaka zilizochakatwa yanazidi kukua ndani pamoja na nje ya nchi. Soko lipo katika nchi jirani kama vile Burundi, Kongo, Rwanda, Kenya, Sudani ya Kusini na Uganda.  Wawekezaji wanakaribishwa kuchakata nafaka pamoja na kuzifungasha ili kuboresha usalama wa chakula na lishe, na kuchichea biashara Maeneo kwa ajili ya Uwekezaji  Mikoa ya Dodoma, Mwanza, Manyara, Mara, Simiyu, Ruvuma, Katavi, Tanga, Songwe na Kilimanjaro Msaada uliopo  Tanzania imekusudia kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo 2025. Uwekezaji hasa katika kuchakata mazao ya kilimo na mifugo ni kipaumbele kikubwa cha Taifa na mazingira wezeshi yanazidi kuboreshwa. 6. VIFUNGASHIO Muhtasari wa Fursa Mambo Muhimu  Kiasi kikubwa cha uharibifu wa chakula nchini ni kwa sababu ya ukosefu wa vifungashio stahiki. Kuwekeza katika uzalishaji wa vifungashio ni fursa ya wazi na itasaidia kuwa na utoshelevu wa chakula pamoja na kuondoa umaskini.  Kwa sasa vifungashio vilivyopo kwa kiasi kikubwa havikidhi ubora wa masoko mbalimbali. Kuna fursa kubwa ya kuzalisha vifungashio kama vile mifuko maalum (multi-layered storage bags e.g PICS).  Vifungashio vitatoa fursa ya kutangaza jina la biashara na hivyo kuongeza ushindani wa bidhaa zinazozalishwa. Maeneo kwa ajili ya Uwekezaji  Mikoa ya Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Kagera, Ruvuma, na Dodoma Msaada uliopo  Mikoa na Halmashauri zote Tanzania wanauhitaji wa vifungashio na wako tayari kupokea wawekezaji katika eneo hili ili kusaidia Taifa katika utekelezaji wa mkakati wa kukuza viwanda nchini.  Kila mkoa umeandaa mazingira wezeshi ya uwekezaji katika viwanda 7. CHAKULA CHA MIFUGO NA SAMAKI Muhtasari wa Fursa Mambo Muhimu  Hili ni eneo linalohitaji kuendelezwa maana kuna uhitaji mkubwa wa chakula cha mifugo na samaki  Tanzania in malighafi nyingi kwa ajili ya uzalishaji wa chakula cha mifugo na samaki kama vile mtama, mahindi, choroko, alizeti nk.  Wawekezaji wanakaribishwa kuzalisha chakula cha mifugo na samaki hasa walenge chakula cha ng’ombe, kuku, samaki nk. Maeneo kwa ajili ya Uwekezaji  Mikoa ya Dodoma, Mwanza, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Ruvuma, na Kagera Msaada uliopo  Viwanda ni kipaumbele cha Taifa ili kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025. Uwekezaji hasa katika kuchakata mazao ya kilimo na mifugo ni kipaumbele kikubwa cha Taifa na mazingira wezeshi yanazidi kuboreshwa. 

No comments:

Post a Comment