Tuesday, May 26, 2020

UTAMADUNI WA KABIRA LA WAHAYA NA ZIWA VICTORIA.


Wahaya ni kabila la watu linalopatikana katika Mkoa wa Kagera, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, kandokando ya Ziwa Victoria hadi mpakani kwa Uganda.

Lugha yao ni Kihaya.
Kabila hilo ndilo linalojulikana kuliko yote ya mkoa wa Kagera, ila ndani yake kuna vijikabila vidogovidogo, kama vile Waziba wa Kiziba, Wahamba wa Muhutwe, Wayoza na Waendangabo wa Bugabo, Wanyaiyangilo wa Muleba, Wasubi wa BiharamuloWalongo wa Geita. Wengine wanawahesabu mle pia Wanyambo wa Karagwe na Kyerwa.
Tofauti kati ya vijikabila zinatambulika kutokana na mabadiliko madogo madogo tu ya maneno na pia lafudhi ya Kihaya ya hiyo sehemu, chakulangoma za asili, majina ya asili.
Mfano: Viazi vitamu (Kiswahili) = ebitakuli (Kiziba) = enfuma (Kihamba, Kiyoza na Kinyaihangilo)
Wahaya ni maarufu kwa uzalishaji wa ndizi na kahawa. Ni kabila ambalo hupenda sifa, kujisifu na kusifiwa. Pia kabila hilo halitasahaulika kwa jinsi walivyopata shida mwaka 1978 kutokana na vita vya Kagera.
Elimu: kuingia kwa wamisionari katika karne ya 19 ambao walianzisha shule nyingi za awali na za kati ambapo ilibidi mtu abatizwe ili aweze kupata elimuWazazi wengi walipeleka watoto wao kubatizwa na hapo kukaanza mvutano, sababu wamisionari walikuwa Wakatoliki kutoka Ufaransa na Uswisi na Walutheri kutoka Ujerumani na Uholanzi. Ndipo kukaanza mashindano ya kuanzisha shule nyingi ili kupata waumini wengi.
Wamisionari pia wakawa mstari wa mbele kufungua hospitali nyingi kila wilaya na vyuo vya ufundi.
Ndiyo maana maeneo hayo ya Kagera elimu ni ya juu kwa wakazi wake na huduma za afya kuliko mikoa jirani. Na kilimo cha kahawa kiliwapa wenyeji fedha za kujenga nyumba bora na kupeleka watoto wao kwenye elimu ya juu zaidi. Pia kulianzishwa chama cha ushirika cha mkoa ambacho kilianzisha shule za watoto wa wakulima kuwasomesha na kutoa mikopo. Eneo hilo lilizidi kurutubishwa kushinda maeneo mengine mengi ya nchi kutoa Uchagga.
Pia wamisionari walianzisha seminari na chuo cha kutoa mapadri wao wenyewe.
Waarabu walioleta Uislamu walikuwa wanakazania sana biashara, si shughuli za maendeleo ya watu.

No comments:

Post a Comment