MACHACHE USIYOYAJUA KUHUSU UTAMADUNI WA MTANZANIA
Jump to navigationJump to searchUtamaduni ni mfumo wa maisha ya watu jinsi wanavyoishi na maendeleo yao kijamii, kiuchumi, kisiasa n.k. Tanzania ni moja kati ya nchi zinazosifika duniani kwa kulinda maadili yao. Kuna makabila yasiyopungua 120 ambayo yote hutunza mila na desturi zao kwa kiasi tofautitofauti.
Mambo yanayofanya Tanzania kutunza utamaduni wake ni haya: heshima iliyopo miongoni mwa jamii hii husaidia watu kuwa na maendeleo kwa sababu ya heshima hiyo.
Nyingine ni utunzaji wa watoto, wazee, vijana pamoja na walemavu ambao wote ni mazao ya jamii ambapo kila mtu katika jamii hufunzwa kuwahudumia watu waliopo katika jamii yake.
Tatu ni mavazi ya heshima ambayo kila mtu anapaswa kuvaa na si mavazi yanayovunja maadili ya taifa.
Uwajibikaji miongoni mwa wanajamii katika shughuli za kijamii ambazo husaidia kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla hivyo jamii ndiyo nguvu kazi katika nchi hasa nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment