Tuesday, May 26, 2020

AFRIKA NA UTAMADUNI WA WAAFRIKA


Jump to navigationJump to seaUtamaduni wa Afrika unajumuisha tamaduni zote ambazo ziliwahi kuweko katika bara la Afrika.


Dhana ya utamaduni wa Afrika nzima ilijadiliwa kwa makini katika miaka ya 1960 na 1970 katika muktadha wa harakati ya Négritude, lakini imepoteza mtindo katika masomo ya Afrika.

Mpasuko mkuu ni kati ya Afrika ya Kaskazini (pamoja na Chad na Pembe la Afrika), ambayo ni sehemu ya ulimwengu wa Kiislamu, na Afrika ya kusini kwa Sahara, ambayo imegawanywa katika idadi kubwa ya tamaduni za kikabila, zikiwemo za Niger-Congo (sanasana za Kibantu), Nilo-Saharan katika maeneo ya Sahara na Sahel na sehemu za Afrika ya Mashariki na Khoisan (wazawa wachache wa Tanzania na Kusini mwa Afrika).

Uenezi mpana wa Kibantu unaojumuisha maeneo ya Afrika ya MagharibiAfrika ya MasharikiAfrika ya Kati na vilevile Afrika ya Kusini, ni matokeo ya uenezi wa Wabantu katika milenia ya 1 BK. Utumizi mpana wa Kiswahili kama lingua franca unaonyesha zaidi athari ya Kibantu juu ya utamaduni wa "Afrika nzima".

Watu[hariri | hariri chanzo]

Asili ya wakazi wengi wa Afrika ni kuwa wazawa.

Afrika ina makabila mengi ambayo hayawezi kuhesabika, na vikundi vya kikabila na vya kijamii. Baadhi ya vikundi hivi vinaashiria wakazi wengi ambao ni mamilioni ya watu. Vingine ni vikundi vidogo vya watu elfu kadhaa. Baadhi ya nchi zina zaidi ya makabila 20 tofauti, na ni tofauti sana katika imani.

Lugha[hariri | hariri chanzo]


Kati ya lugha maarufu zaidi zinazozungumzwa ni
 Kiarabu, Kiswahili na Kihausa. Nchi chache za Afrika hutumia lugha moja na kwa sababu hii, lugha rasmi kadhaa zinatumika, za Kiafrika na za kutoka nje. Baadhi ya Waafrika pia wanaweza kuzungumza lugha mbalimbali kama vile Kimalagasi, Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kihispania, Kibambara, Kisotho na nyinginezo.Bara la Afrika lina mamia ya lugha, na kama lahaja zinazozungumza na makabila tofauti zinajumuishwa, idadi ni kubwa zaidi. Kupitia makadirio mengi, Afrika ina zaidi ya lugha elfu. Lugha na lahaja hizo zote hazina umuhimu sawa: baadhi huzungumzwa na watu mia chache tu, nyingine huzungumzwa na mamilioni.

Lugha za Afrika huonyesha umoja wa tabia na vilevile utofauti. Familia nne kuu na maarufu za lugha za kienyeji ni:

Senta ya mapema ya maandiko ilikuwa African Ink Road.

Pamoja na nchi chache mashuhuri katika Afrika ya Mashariki, karibu nchi zote za Afrika zilisiliki lugha rasmi zilizoasilika kutoka nje ya bara na kuenea kupitia ukoloni au uhamiaji wa binadamu. Kwa mfano, katika nchi mbalimbali, Kiingereza na Kifaransa hutumiwa kwa mawasiliano katika nyanja za umma, kama vile serikalibiasharaelimu na vyombo vya habariKiarabuKireno na Kiafrikaans ni mifano la lugha zisizo za asili ya Kiafrika ambazo hutumika na mamilioni ya Waafrika leo, katika nyanja za umma na za binafsi. Tofauti ni Kimalagasi kisiwani Madagaska, ambako Waafrika walihamia kutoka barani wakikuta wenyeji kutoka Indonesia.

Sanaa na Afrika[hariri | hariri chanzo]

Afrika ina mila tajiri ya sanaa [1]Sanaa za Afrika hujieleza katika aina mbalimbali za uchongaji wa mbaoshaba na matendo ya sanaa ya ngozi. Sanaa ya Afrika pia inajumuisha uchongaji, uchorajiufinyanzimavazi ya mwili na ya kichwa katika sherehe na mikutano ya kidini.

Utamaduni wa Afrika daima umetilia mkazo vile mtu anavyojitokeza na johari zimebaki vidude muhimu ya kibinafsi. Vipande vingi vya johari vimetengenezwa na simbi au vifaa kama vya simbi. Vilevile, miundo ya maskhara zinatengenezwa kwa umakini na ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Afrika. Maskhara hutumika katika sherehe mbalimbali kuashiria mizimu na vizuka, wahusika katika hadithi na miungu.

Katika mila nyingi ya sanaa ya Afrika, baadhi ya mandhari adhimu kwa utamaduni wa Afrika hujirudia kama vile wapenzi wawili, mwanamke na mtotomume na silaha au mnyama, na mtu kutoka nje au mgeni. Wapenzi wawili wanaweza kuwakilisha mizimu, mwanzilishi wa jamiiwapenzi wawili waliooana au mapacha. Mandhari ya wapenzi wawili adimu huonyesha undani wa wanaume na wanawake. Yule mama na watoto au watoto hufumbua hamu kubwa ya wanawake wa Afrika kupata watoto. Mandhari pia inaashiria mama mirihi na watu kama watoto wake. Mandhari ya mtu na silaha au mnyama inaashiria fahari na nguvu. Mgeni anaweza kuwa ametokea kutoka baadhi ya makabila au awe mtu kutoka nchi nyingine, na zaidi upotovu wa mgeni huonyesha pengo kubwa kutoka kwa mgeni.

Fathi Hassan anachukuliwa kama mwakilishi wa sanaa ya kisasa ya Afrika.

Folklore na dini ya kimila[hariri | hariri chanzo]

Kama tamaduni zote za binadamu, "Folklore" ya kiafrika na masimulizi huashiria pande mbalimbali za utamaduni wa Afrika [2]. Kama karibu staarabu na tamaduni zote, hadithi za mafuriko zimekuwa zikienea katika maeneo mbalimbali ya Afrika. Kwa mfano, kulingana na hadithi ya chuchu au Mtwakinyonga aliposikia kelele ya ajabu akiwa mtini, shina la mti huo ulifunguka na maji ilimwagika kama gharika kuu iliyoenea kote ardhini. Wapenzi wa kwanza wa binadamu waliibuka kutoka majini. Vilevile, hadithi moja kutoka Cote d'Ivoire inasema kwamba mhisani mmoja alipatiwa kila kitu alichokuwa nacho. Mungu wake, Ouende , alimtuza kwa kumpa utajiri, alimshauri aondoke kutoka eneo hilo, na alituma miezi sita ya mvua kuharibu jirani wake wachoyo.

Upishi[hariri | hariri chanzo]

Afrika ni bara kubwa na vyakula na vinywaji vyake hudhaniwa mivuto ya kienyeji, na utumizi wa vyakula vya kikoloni vya kimila, vikijumuisha pilipilinjugu na mahindi, vilivyoanzishwa na wakoloniUpishi wa Afrika ni mchanganyiko wa matunda na mbogamaziwa na bidhaa za nyama. Mlo wa kijiji cha Afrika mara nyingi huwa maziwa na bidhaa za maziwa. Wanyama na samaki hukusanywa katika eneo kubwa la Afrika.

Upishi wa kimila wa Kiafrika ina tabia ya utumizi wa wanga kama umakini, ikifuatwa na kitoweo chenye nyama au mboga, au yote mawili. Mihogo na viazi vikuu ndizo mboga kuu. Waafrika pia hutumia mboga zilizopashwa moto na ambazo zina pilipili. Vyakula vya mboga vilivyopashwa moto au kuchemshwa, mbaazimaharagwe na nafaka, mihogo, viazi vikuu na viazi vitamu huliwa kwa wingi. Katika kila eneo la Afrika, kuna aina mbalimbali za matunda ya pori na mboga ambazo hutumika kama chakula. Mtengomaji na ndizi ni baadhi ya matunda yanayojulikana.

Tofauti hujulikana katika tabia za kula na kunywa barani Afrika. Hivyo, Afrika Kaskazini, pamoja na Mediteranea kutoka Moroko hadi Misri zina tabia tofauti za chakula kuliko Waafrika wa Sahara ambao hula mlo wa kujikimu. Nigeria na sehemu za pwani za Afrika Magharibi hupenda vyakula vya pilipili. Idadi ya Waafrika ambao si Waislamu pia hutumia vileo, ambavyo huenda vyema na vyakula vingi vya Kiafrika. Pombe inayojulikana sana ndani ya Afrika ni mvinyo kutoka Ethiopia inayoitwa Tej iliyotengenezwa kwa kutumia asali.

Mbinu za kupika za Afrika Magharibi mara nyingi kuchanganya samaki na nyama, pamoja na samaki iliyokaushwa. Upishi wa Afrika Kusini na nchi jirani kwa kiasi kikubwa zinapika vyakula vya machanganyiko, kwa kupata mvuto kutoka wahamiaji kadhaa ambao ni pamoja na Wahindi ambao walileta supu ya adesi(dals) na mchuziMalays waliokuja na michuzi yao ya viungo, na Wazungu na "mixed grills" ambao sasa inajumuisha nyama ya wanyama wa Afrika.

Kimila, vyakula vya Afrika Mashariki ni tofauti kwa maana kwamba bidhaa za nyama haviko kwa ujumla. Ng'ombekondoo na mbuzi walichukuliwa kama aina ya sarafu, na kwa ujumla wanyama hao hawatumiwi kama vyakula. Mivuto ya Kiarabu inajitokeza katika upishi wa vyakula vya Afrika Mashariki - mchele uliopikwa kwa viungo katika mtindo fulani, matumizi ya karafuumdalasini na viungo vingine vingi, na juisi.

Waethiopia wanadai kuwa wa kwanza kulima kahawa, na wana sherehe za aina nyingi za kahawa, kama sherehe ya chai ya Kijapani. Kutoka Ethiopia, kahawa ilienea Yemen, kutoka huko ilienea Arabia, na kutoka huko ikaenea duniani kote.

No comments:

Post a Comment