Thursday, June 4, 2020

UTAMADUNI NA MAENDELEO YA TANZANIA

Nchi ya Tanzania ilizaliwa mwaka 1964 baada ya Tanganyika na kisiwa cha Zanzibar kuungana chinia ya serikali mmoja. Julius K Nyerere (Kiongozi mkuu wa TANU) na Abeid Amana Karume (Kiongozi mkuu wa ASP) ndio walioongoza muungano huu.

Siasa na Ukoloni

Karne kadhaa kabla ya mwaka huu, Tanganyika ilikuwa koloni ya Urenu kuanzia karne ya 15 had ya 17, ambapo Sultan wa Oman akashika nchi. Baada ya hapo, Ujerumani iliongeza Tanganyika katika orodha yake ya wakoloni mpaka Vita Kuu 1. Baada ya hapo, Uingereza uliiweka chini ya uongozi wa Shirikisho la Mataifa. Hata hivyo, Taganyika ilipata uhuru wake Desemba 9 mwaka 1961 kutoka kwa ukoloni wa Waingereza. Ila, chakushangaza kidogo ni kwamba siku hii ndio iliyokubalika kama siku ya uhuru ya Tanzania, wakati Tanzania haikuwepo had Aprili 26th 1964.

Ingawa matukio haya ni muhimu katika historia ya Tanzania, kuna mengine kama:

1967 – Kwenye Maadhimisha ya Arusha, Nyerere alianzisha rasmi mchakato wa ujamaa na uchumi wa kujitegemea

1977 – Chama Cha Mapinduzi linaundwa baada ya TANU na ASP kuungana.

1978 – Majeshi ya Uganda yanaingia na kutawala kipande cha nchi.

1979 – Majeshi ya Tanzania yanaingia Uganda, yakikamata Kampala, mji mkuu, na kusaidia kumtoa Rais Idi amin

1985 – Nyere anastaafu na Rais wa Zanzibar, Ali Hassan Mwinyi, anakuwa Rais wa Tanzania.

1992 – Katiba inarekebishwa kuruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa

1995 – Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi unafanyika

Historia ya Kiasili na Utamaduni

Olduvai Gorge

Kuna uhusiano gani kati ya mkonge na Olduvai Gorge? Zote zipo kwenye maeneo ambapo ushaidi wa mababu wa kwanza kwa binadamu, upo. Jina la Olduvai Gorge, ambayo ni ukosefu wa kuandika Oldupai ambayo ni jina la mimea ya mkonge yanayoota hapo, uligunduliwa na Loui na Mary Leakey kati ya miaka ya 1930 – 1950. Sasa, hii inamaanisha kwamba mababu ya binadamu walikuwa watanzania? Huwezi jua!

Makabila  

Tanzania ina zaidi ya makabila 120 na ilipata uhuru bila damu kumwagika.

Kati ya makabila haya, 4 zinajulikana zaidi ya zingine kwa zababu tofauti, zikiwemo:

  • Wasukuma, kabila kubwa zaidi Tanzania
  • Wachagga, kabila inayojulikana kwa kufanya biashara
  • Wamakonde, kabila inayojulikana kwa vinyago vya mbao
  • Wamasai, wapiganaji hodari na wafugaji.

Lugha

Kiswahili ni mchanganyiko wa lahaja za kibantu pamoja na kiarabu. Nyerere alikuwa mpiga debe mkubwa wa Swahili na ikawa lugha ya taifa ya Tanzania. Hii imesaidia kuweka umoja kwenye nchi ilio na zaidi ya kabila 120, zote zikiwa na lugha yao.

Salamu na kusalimiana ni kitu muhimu kwenye utamaduni wa Tanzania. Iwe unaingia ofisini, umeenda dukani au unakutana na marafiki, kusalimiana na ulionao au walio karibu nawe ni muhimu. Pia, ‘Jambo’ sio salamu inayotumika Tanzania. Salamu ya kawaida ni Habari/Habari yako/Habari za saa hizi. Salamu zisizo rasmi ni kama Mambo/Mambo vipi?/kwema?/ Salama?

Nguo na Vitambaa Asili

Tanzania ina aina mbili za mavazi zinazojulikana kokote nchini.

Kanga ni kitambaa cha pamba linalo valiwa na wanawake, iki fungwa kiunoni kwenda chini. Asili yake ni ni kutoka wanawake wa Zanzibar katika karne ya 19. Ni nyepesi, yenye rangirangi na inamatumizi mengi kama taulo, scafu ya kichwani na mengineyo. Umaarufu wake umekuwa na siku hizi ni kawaida kukuta methali ikiwa imeandikwa kwenye kanga.

Kitenge,ina rangi kali na nzitu zinazoendana na michoro yaliyomo. Tofauti kubwa kati ya kitenge na n kanga ni kwamba kitenge ni nzito zaidi. Pia, siku hizi bukta, mashati na t-shirt za kitenge zimeenea mjini. Zaidi ya hapo, mitindo ya vitenge vimeanze kuonekana kwenye dunia ya mitindo na mavazi.


Jiografia

Tanzania inajisifia sana kwa kuwa ina Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kuliko zote Africa na Ziwa Viktoria, ziwa inyokwenda chini kuliko yote. Kuelewa ukubwa wa Tanzania vizuri, iko mpakani na Kenya na Uganda (Kaskazini); Burundi, Rwanda na DRC (Magharibi) na Msumbiji, Zambia na Malawi (Kusini). Ongezea bahari la India lilo pwani, na utaanza kuelewa ukubwa wa Tanzania.

Ukipata muda, funga safari za kwenda Kilimanjaro kutoka Dar es Salaam ukisindikizwa na milima ya Usambara, kwa mfano. Kun mengi ya kuona!

Nchi ya Amani

Kuanzia siasa na watu wake, ardhi na lugha, historia ya Tanzania ina mambo mengi. Kwa ujumla, watanzania ni watu tulivu wenye heshima na uvumulivu. Nchi hii imetoka mbali na inajiendeleza polepole ila vizuri. Ila kuna matatizo makubwa mbali mbali. Lakini, kwa kifupui nchi inaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment